Asahihisha mitihani akiwa icu na kufariki muda mfupi baadae

Mwalimu amalizia kusahihisha mitihani ya wanafunzi wake akiwa mgonjwa kitandani kabla ya kupelekwa ICU na kufariki.

Mtoto wa mwalimu huyo Sandra Venegas alipiga picha hii ya baba yake akiwa kwenye kitanda cha hospitali. Baba yake alijua kwamba alikuwa akipelekwa (ICU) hivyo alifungua laptop yake na kuhakikisha anamaliza kusahihisha mitihani ya wanafunzi wake na alifariki siku iliyofuata

"Walimu huweka saa nyingi za ziada kwa wanafunzi wao, masaa ambayo wengi hawatambui. Hata wakati wa janga, hata wakati wa shida ya kiafya, walimu wana wasiwasi juu ya kukamilisha majukumu yao, "aliandika mtoto huyo

Share: