Ariel henry ametua puerto rico baada ya kushindwa kurejea nchini mwake

uwanja wa ndege katika mji mkuu Port-au-Prince, umefungwa.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, aliwasili katika mji mkuu wa San Juan siku ya Jumanne baada ya kuruka kutoka jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Kwa siku chache zilizopita, Bw Henry alikuwa hajulikani aliko kufuatia ziara yake nchini Kenya.

Ghasia nchini Haiti zimeongezeka bila kuwepo kwake, huku magenge yenye silaha yakijaribu kuuteka uwanja wa ndege wa kimataifa ili kumzuia kutua.

Kiongozi wao, Jimmy "Barbecue" Chérizier, amemtaka waziri mkuu kujiuzulu, akionya kwamba nchi hiyo inaelekea "moja kwa moja kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vitasababisha mauaji ya halaiki".

Bw Henry kugeuza njia kutoka kwa taifa analoongoza ni ishara ya jinsi Haiti imekuwa na hali duni katika siku za hivi karibuni.

Haiti sasa inakaribia kuwa taifa lililoshindwa. Ndege ya Ariel Henry ililazimika kuelekezwa Puerto Rico , eneo la Marekani , baada ya kuzuiwa kuingia Haiti na Jamhuri ya Dominika, tovuti za habari za ndani ziliripoti.

Jamhuri ya Dominika Jumanne ilitangaza kuwa inafunga anga yake na nchi jirani ya Haiti, ambayo inashiriki kisiwa cha Hispaniola.

Kiongozi wa nchi hiyo, Luis Abinader, hivi karibuni alisema hatua zitachukuliwa ili kuhakikisha kiwango cha "amani na udhibiti" kinadumishwa katika mpaka wake wa ardhini.

Sababu kadhaa zinaweza kueleza kwa nini ndege ya Bw Henry haikuruhusiwa kutua Haiti, huenda ikawa ilikuwa hatua ya utaratibu.

Tangu hali ya hatari kuwekwa Jumapili, safari zote za ndege zimekatishwa hadi ilani nyingine itakapotolea na uwanja wa ndege katika mji mkuu Port-au-Prince, umefungwa.

Sababu nyingine inaweza kuwa kwa usalama wake mwenyewe. Bw Henry alikuwa shabaha ya wazi kwa magenge ambayo yanamtaka aondoke madarakani, na kurejea kwake katika hatua hii kunaweza kuonekana kuwa kikwazo zaidi kwa utulivu wa taifa, kuliko msaada.

Hofu kubwa kwa waziri mkuu na wafuasi wake, ikiwa ni pamoja na huko Washington, ni kwamba jaribio lake lisilofanikiwa la kurudi nyumbani linamdhoofisha zaidi.

Inatoa hisia kwamba mamlaka zilizo chini yake zinabatilisha nia yake ya kurejea katika ardhi ya Haiti.

Badala yake, ameketi Puerto Rico kutokana na hilo lazima atambue hatua yake inayofuata wakati nchi yake inashuka zaidi kwenye machafuko

Share: