Argentina: rais javier milei amepanga kuwafuta kazi wafanyakazi wa serikali 70,000

Akizungumza Machi 26, 2024 amesema amepanga kusitisha baadhi ya Miradi ya Umma na kufuta zaidi ya programu 200,000 za Ustawi wa Jamii baada ya Miradi hiyo kihusishwa na Rushwa.

Pia Rais Javier Milei amepanga kuwafuta kazi Wafanyakazi wa Serikali 70,000 ambao Mikataba yao inatarajiwa kumalizika hivi karibuni ili kupunguza matumizi ya Serikali

Amesema “Tumeondoa suala la Uhamisho wa kazi na pia tunaondoa Wafanyakazi 70,000 wa Umma. Miradi ya Umma ni chanzo kikuu cha wizi, wizi ambao naamini watu wema wote wanapaswa kupinga.”

Share: