AMEHUKUMIWA ADHABU YA KIFO ,KIONGOZI MKUBWA SEREKALI YA CHINA

Wang Yong, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa serikali ya mkoa unaojiendesha wa Xizang nchini China, amehukumiwa adhabu ya kifo iliyosimamishwa kwa miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kupokea hongo.

Mahakama ya Kati ya Watu ya Chenzhou katika jimbo la Hunan, imesema kuwa kati ya mwaka 2007 na 2023, Wang alitumia nyadhifa zake mbalimbali za uongozi kupokea hongo ya zaidi ya yuan milioni 271. Alitumia madaraka yake kutoa upendeleo kwa mashirika na watu binafsi katika mikataba na maeneo mengine.


Mahakama imesema makosa ya Wang yalikuwa mabaya sana na yalisababisha hasara kubwa kwa maslahi ya nchi na umma.

Hata hivyo, adhabu yake ilionekana kuwa na nafuu kwa sababu alikiri makosa yake, akaonyesha majuto, na akarejesha fedha zote alizopata kwa njia haramu.


Nchini China, hukumu ya kifo iliyosimamishwa kwa kawaida hugeuzwa kuwa kifungo cha maisha jela ikiwa mfungwa ataonyesha tabia njema ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Share: