Aliyewahi kuwa mwenyekiti na mfadhili wa yanga, yusuf manji anatarajiwa kuzikwa leo nchini marekani

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alifariki juzi Jumamosi anatarajiwa kuzikwa leo nchini Marekani.

Manji alifariki akiwa hospitalini Florida Marekani ikiwa ni miezi miwili tangu alipofanya mahojiano marefu na Mwananchi Digital akiwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarita ambayo mtoto wa marehemu Mehbub Manji amelitumia Mwananchi inasema wao kama familia wanashukuru kwa jinsi ambavyo Watanzania wameendelea kuombeleza kifo cha baba yao na jinsi ambavyo wameendelea kumuombea huko alipo.

“Tunawaomba muendelee kumuombea baba yetu awe na safari njema huko aendapo. Alikuwa anaipenda Tanzania na Watanzania wanampenda sana, lakini tunaomba kuwaambia kuwa Manji atazikwa leo saa tisa alasiri Orlando, Florida Marekani, karibu na sehemu aliyozikwa baba yake. Baba tulikupenda lakini Allah amekupenda zaidi. Yusuf Manji: Ni baba, rafiki, kiongozi,” ilimalizia taarifa hiyo.

Share: