Akon ataporwa asilimia 90% ya ardhi ya mji wake na serikali ya senegal asipoendelea na ujenzi wa mji wa ‘akon city’

Mwanamuziki Kutoka New Jersey nchini Marekani mwenye asili ya Senegal akon Ataporwa Asilimia 90% Ya Ardhi Ya Mji Wake Na Serikali Ya Senegal Endapo Asipoendelea Na Ujenzi Wa Mji Huo ‘Akon City’ Alioahidi Kuujenga Tangu 2018 Huko Nchini Senegal. 

Imeripotiwa Kuwa Msanii Huyo Ametumiwa Barua Na Serikali Ya Senegal Ikimtaka Aendelee Na Ujenzi Wa Mji Wake Huo Utakaogharimu Zaidi Ya Tril 16 Kama Walivyokubaliana 2018.


Mwaka 2020 Akon Alitia saini na kampuni ya Sapco kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mji wake ‘Akon City’ ambao watakuwa wakitumia sarafu yake iitwayo Akoin, ukiwa na majengo ya biashara, viwanja vya ndege, Shule na burudani, Lakini Hadi Leo Hii Hakuna Ujenzi Unaoendelea Katika Mji Huo. 

Hata Hivyo Mwanasheria Wa Nyota Huyo Bado Hajasema Chochote. Mmoja Kati Ya Watu Wa Akon Amedai Kuwa Hawakuwa Na Taarifa Kuhusu Barua Hiyo. Lakini Pia Kampuni Ya Sapco Iligoma Kutoa Taarifa Zaidi Juu Ya Hilo. 

Kutokuendeleza Ujenzi Wa Mji Huo Umewakatisha Tamaa Wakazi Wa Senegal Ambao Waliahidiwa Kupata Ajira, Hospitali, Vyuoni, N.k.

Share: