Akiri kumsingizia mtu ambaye hamjui kesi ya kumbaka na kumfunga.

Mwanamke Mmarekani kutoka Pennsylvania alikiri kuwa alimshitaki kwa uwongo Mwanaume asiye na hatia ambaye hajawahi kumwona kwa madai ya kujaribu kumbaka na kumteka nyara.

Anjela Borisova Urumova, mwenye umri wa miaka 20, alikiri mashtaka ya kutoa ripoti ya uwongo kwa polisi dhidi ya Daniel Pierson, mwenye umri wa miaka 41, ambaye alimshtumu kwa kujaribu kumteka nyara na kumbaka.

Pierson alishikiliwa kwa dhamana ya dola milioni moja, alishtakiwa kwa makosa kadhaa ya jinai, na alitumia mwezi mmoja gerezani kutokana na madai hayo ya uwongo.

Kulingana na Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Bucks County, Urumova alidai kuwa mnamo Aprili 16, 2024, Pierson alimshambulia nje ya duka kubwa la rejareja.

“Kwa mujibu wa uchunguzi, Polisi wa Middletown Township walikusanya na kupitia video za ulinzi zilizopatikana kutoka kwa maduka kadhaa eneo la tukio lililoripotiwa, na mpelelezi kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Wilaya ya Bucks alifanya uchunguzi wa kielektroniki wa data ya simu ya mkononi ya Urumova,” ofisi ya mwendesha mashtaka ilisema katika taarifa.

Urumova alikabiliwa na mamlaka na alikiri kuwa alidanganya kuhusu tukio zima, akithibitisha kuwa hakuwa ameshambuliwa na mtu yeyote, walisema waendesha mashtaka.

Share: