Ahadi za kupunguza uzalishaji wa hewa chafu hazitekelezeki

Shirika la ufuatiliaji wa hali ya hewa limeonya kuwa nchi ambazo zimeahidi kufikia lengo la kutokomeza uzalishaji wa hewa Chafu.

Shirika la ufuatiliaji wa hali ya hewa limeonya kuwa nchi ambazo zimeahidi kufikia lengo la kutokomeza uzalishaji wa hewa chafuzi, hazijatangaza mipango yoyote ya kuachana na matumizi ya nishati ya mafuta ya visukuku.

Kutokana na hilo, shirika hilo limesema ahadi hizo huenda zikashindwa kutekelezeka. Ripoti mpya ya shirika la "Net Zero Tracker" imetolewa huku kukiwa na majadiliano yenye utata katika mazungumzo ya hali ya hewa ya COP28 huko Dubai hasa kuhusu ikiwa kama mataifa yatakubali kupunguza au kuachana kabisa na nishati ya mafuta ambayo inasababisha ongezeko la joto duniani.  

Ripoti hiyo imeendelea kuwa, karibu nchi 150 ziliahidi kufikia lengo la kutozalisha hewa chafu ambayo inajumuisha asilimia 88 ya gesi chafuzi inayozalishwa duniani kote kutokana na shughuli za binadamu.

Share: