AFYA: Brazil kushirikiana na zanzibar katika mradi wa kupunguza vifo vya mama na mtoto

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameishukuru Serikali ya Brazil kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mradi wa kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa hospitali za Unguja na Pemba.


Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa wataalamu kutoka Wizara ya Afya ya Brazil na wakala wa ushirikiano wa ufadhili wa Brazil (ABC), waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 26 Juni 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Zanzibar ipo tayari kujifunza uzoefu kutoka Brazil kuhusu kuboresha huduma za afya ikiwemo watoto njiti , kupunguza vifo vya mama na mtoto, na kuwajengea uwezo kwa wafanyakazi wa sekta ya afya.


Ujumbe huo umeambatana na Mwakilishi wa Heshima wa Brazil Zanzibar, Abdulsamad Abdulrahim na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mhe.Nassor Mazrui.

Share: