Afrika kusini inaitaka mahakama kuu kuiamuru israel kusitisha mashambulizi yake ya kijeshi katika mji wa rafah

Israel itatoa majibu yake katika mahakama siku ya Ijumaa

Afrika Kusini inaitaka mahakama kuu ya Umoja wa Mataifa kuiamuru Israel kusitisha mashambulizi yake ya kijeshi katika mji wa Rafah kusini mwa Gaza.

Inawasilisha kesi yake kusikilizwa kwa siku mbili katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) huko The Hague.

Israel itatoa majibu yake katika mahakama siku ya Ijumaa.


Afrika Kusini pia inataka kulazimisha Israel kuruhusu wafanyakazi wa misaada, waandishi wa habari na wachunguzi "kuingia Gaza bila vikwazo'' .

Tayari mahakama hiyo inazingatia kesi iliyowasilishwa mbele yake na Afrika Kusini mwezi Januari ikiishutumu Israel kwa kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Israeli iliyataja madai hayo kuwa ya uwongo na "yamepotoshwa sana".

Israel ilianza mashambulizi yake dhidi ya Hamas mjini Rafah siku 10 zilizopita, huku kukiwa na onyo kutoka kwa Umoja wa Mataifa na mengine kuhusu hatari kubwa inayowakabili raia.

Zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao walikuwa wakikimbilia Rafah na karibu 600,000 wamekimbia kutoka hapo tangu kuanza kwa operesheni hiyo.


Ombi la Afrika Kusini kwa mahakama hiyo linaishutumu Israel kwa kutekeleza oparesheni za "mauaji ya halaiki" huko Rafah na kwingineko huko Gaza, na inasema kwamba "lazima iagizwe kukomesha".

Akihutubia mahakama mwanzoni mwa kusikilizwa kwa kesi hiyo, wakili wa Afrika Kusini Vaughan Lowe KC alisema kwamba "ushahidi wa uhalifu wa kutisha na ukatili unaharibiwa kihalisi na kuonewa, na hivyo kuwafuta wale ambao wametenda uhalifu huu na kufanya dhihaka. ya haki".

Share: