Abdulrahman Kinana: Mengi yatasemwa kuhusu hayati mzee ali hassan mwinyi

Mengi yamesemwa na mengi yatasemwa kuhusu marehemu Rais wetu wa awamu ya pili mzee Ali Hassan Mwinyi.

"Mimi nizungumze mambo mawili. La kwanza, Sote ni mashahidi kwamba Rais Mwinyi alifanya kazi kubwa sana ya kulitoa taifa letu kutoka kwenye chama kimoja kwenda kwenye mfumo wa vyama vingi.

"Jambo hili halikuwa jambo dogo na halikuwa jambo rahisi. Alilitoa taifa letu kwenye uchumi ambao ambao ulikuwa mikononi mwa serikali kuwa uchumi huria uliotoa nafasi kwa kampuni na mashirika binafsi kufanya shughuli zao katika taifa letu"

Mambo yote hayo hayakuwa rahisi hasa ukizingatia haya yote aliyafanya wakati waasisi wa taifa letu baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa hai.



Mzee Mwinyi alifanya kazi kubwa ya kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kwakuwa karibu sana na baba wa taifa na kila uamuzi alioutoa ulikuwa ni uamuzi uliomshirikisha baba wa taifa na wote waliridhia kwa pamoja.

Nichukue nafasi hii kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kutoa pole nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa uongozi wa taifa letu,kwa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar, kwa mama Sitti na familia yote ya Mzee Mwinyi na tumuombee kwa Mwenyenzi Mungu amfungulie milango ya pepo na amsamehe madhambi yake."

Abdulrahman Kinana: Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa


Share: