Muandaaji wa filamu nchini Somalia, Ahmed Farah amewamwaga waongozaji wa filamu Tanzania baada ya kushinda Tuzo za Kimataifa za Filamu ‘ZIFF’ 2024 zilizotolewa Ngome Kongwe Zanzibar.
Ahmed kupitia filamu yake ya Arday ameshinda Tuzo ya ZIFF 2024 katika kipengele cha tamthilia bora ya Afrika Mashariki. Kipengele hicho kilishindaniwa na tamthilia za Tanzania kama vile Jua Kali ya Leah Mwendamseka, Jacob Stephen (Report), Simon Cherehani (Twisted) , Ramadhan Said (Bunji) na Florence Mkinga (Dhohar).
Hata hivyo tamthilia za mataifa mengine zilizowania kipengele hicho ni kutoka Uganda (Sanyu) iliyoongozwa na Mathew Nabwiso, Allan Manzi (Junior Drama Club) na (Damalie ) Don Mugisha kwa upande wa Kenya (Volume) iliyoongozwa na Tosh Gitonga.
Tuzo hizo zimetolew Agosti 4, 2024 Kisiwani Unguja kwenye ukumbi wa Ngome Kongwe.