Jambo hili lenye mafanikio makubwa limeleta matumaini kwa wanaotegemea kupokea figo kwa wakati ufaao kabla ya kuzidiwa na ugonjwa na kupata tiba bora ya ugonjwa wa figo
Mgonjwa aitwae Richard Slayman (62) aliyepandikizwa figo ya Nguruwe iliyobadilishiwa vinasaba, ameruhusiwa kutoka hospitalini ikiwa ni siku kadhaa tu toka alipofanyiwa upasuaji huo March 2024 katika Hospitali Kuu ya Massachusetts (MGH) Boston, Marekani ukiwa ni upasuaji wa kwanza duniani wa aina yake.
Mwanaume huyo aliugua ugonjwa ambao ulifanya figo zake kushindwa kufanya kazi kikamilifu kwa kujitegemea pamoja na ugonjwa wa kisukari ndipo ikilazimika kupandikizwa figo mpya ambapo alipokea figo mpya mwaka 2018 lakini baada ya muda iliacha kufanya kazi.
Upasuaji huu wa March umeamsha matumaini makubwa ya kuwapandikizia Binadamu viungo vya Wanyama ‘xenotransplantation’ kitendo ambacho kinaweza kutatua uhaba wa viungo kutoka kwa Binadamu katika ngazi ya kimataifa kwani kwa bahati mbaya hakuna figo za kutosha, amesema Dk Leonardo Riella, Mkurugenzi wa Matibabu ya Upandikizaji wa Figo.
Jambo hili lenye mafanikio makubwa limeleta matumaini kwa wanaotegemea kupokea figo kwa wakati ufaao kabla ya kuzidiwa na ugonjwa na kupata tiba bora ya ugonjwa wa figo ambapo Figo aliyopokea Slayman ilirekebishwa na kuwekwa sawa na kampuni ya ‘eGenesis’ yenye Makao yake Makuu Massachusetts, Marekani ambapo Hospitali hiyo imesema Richard yuko vizuri na hatohitajika kufanyiwa tiba ya ‘dialysis’.
Imeelezwa kuwa zaidi ya Watu 100,000 nchini Marekani wanasubiri upandikizaji wa viungo ambapo takwimu zinaonyesha takriban Watu 17 hupoteza maisha kila siku wakisubiri kupandikizwa viungo huku figo kikiwa kiungo kinachohitajika zaidi kwa njia za upandikizaji