Youngthug kusaidia watu wenye uhitaji baada ya kutoka jela
Baada ya usiku wa jana rapper kutoka Marekani Jeffery Williams maarufu kama YoungThug kuachiliwa huru na kupunguziwa adhabu ya kifungo, rapper huyo wa Atlanta kupitia watu wake wa karibu ametajwa kuwa kwenye mipango wa kufanya tamasha la mwaka la kusaidia watu wenye uhitaji mara tu atakapo kaa sawa uraiani.
Ikumbukwe kuwa msanii huyo YoungThug alikiri makosa sita, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika shughuli za genge la uhalifu mitaani, huku akipewa masharti kama ya kutowasiliana na Washtakiwa wenzake zaidi ya ndugu zake na msanii wake GUNNA.
Share: