Yemi alade, familia inanilazimisha niolewe

Msanii wa Nigeria Yemi Alade Amefichua kwamba mara kwa mara anakumbana na shinikizo kutoka kwa familia na marafiki kuolewa na kupata watoto.

Licha ya uvumi ulioenea wa ndoa yake na meneja wake, yemi Alade aliweka

wazi hali yake ya uhusiano kwa kusema kwamba wakati ukifika nitaingia kwenye ndoa na kupata mtoto.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Cool FM, Yemi Alade alisema

"Shinikizo la familia ni jambo gumu kupinga kwa sababu linatokana na watu ninaowaheshimu, wakisisitiza kwamba ninafaa kuolewa, hata hivyo ninaamini kwamba ikiwa kwa kweli wana nia njema, watanivumilia kwa sababu kupata mwenzi anayefaa ni muhimu zaidi kuliko kuolewa tu."

Lakini zaidi ya hayo, sidhani kama mtu yeyote anapaswa kuharakisha kufanya uamuzi mbaya wa kuwa na mwenzi asiye sahihi. 

Share: