Wimbo wa zuchu "sukari" wafikisha views milioni 100 youtube

Msanii wa kike kutoka Label ya wcb wasafi ameandika historia kwenye muziki wake baada ya wimbo wake 'Sukari' kufikisha views zaidi ya Milioni 100 kwenye mtandao wa youtube wimbo ambao hajashirikiana na msanii yeyote Afrika mashariki

Zuchu ameshare furaha yake hiyo na mashabiki kwa kuweka kipande kidogo cha wimbo huo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwashukuru mashabiki pamoja na wale wote waliofanikisha project yake hiyo

Ungependa kuona msanii gani mwingine wa kike kutoka Tanzania akifikia mafanikio haya makubwa?

Share: