Wimbo wa "maelekezo chapter 3" wa msanii moni centrozone warudishwa youtube

Msanii maarufu wa muziki wa hip hop hapa nchini, Moni Centrozone ametoa taarifa muhimu kuhusu wimbo wake wa "Maelekezo Chapter 3" kupitia akaunti yake ya Instagram leo.

Kupitia ujumbe wake, Moni Centrozone amefichua kwamba miezi mitano imepita tangu aliposhusha video ya wimbo huo kwenye YouTube. Hata hivyo, leo amepokea habari njema kwamba malalamiko yaliyokuwepo yamefutwa na mtu aliyelalamika. Hii inamaanisha kwamba wimbo huo umepata nafasi ya kuwekwa tena mtandaoni.

Kufuatia hatua hiyo, Moni Centrozone ameamua kuweka upya video hiyo kwenye mtandao wa YouTube. Hata hivyo, hakuwa na matarajio makubwa kwamba video hiyo ingeweza kufikia kiwango cha kutrend tena.

Akizungumzia uamuzi huo, Moni Centrozone ameeleza kwamba "hii ni moja ya miradi yangu kubwa na ninayoipenda sana. Imenifuta machozi baada ya miezi mitano. Kiteknolojia ni kama kazi mpya jijini. Asanteni sana kwa upendo wenu."

Wimbo wa "Maelekezo Chapter 3" sasa unategemewa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha nyimbo maarufu huku Moni Centrozone akiendelea kuwavutia mashabiki wake na kazi zake zenye ubunifu mkubwa katika tasnia ya muziki wa hip hop.

Share: