Wimbo wa komasava wa diamond platnumz wazidi kwenda kimataifa baada ya kuonekana wasanii na watu mashuhuri dunia wakiucheza

Ngoma mpya ya Diamond Platnumz, Komasava imeendelea kuteka mioyo ya mashabiki dunia na sasa supastaa wa Marekani, Chris Brown ameonekana akicheza wimbo huo kupitia mtandao wa TikTok.

Hata hivyo, mtayarishaji wa ngoma hiyo Salmin Maengo ‘S2KIZZY’ ameeleza kuwa wimbo huo ambao Diamond amemshirikisha Chley na Khalil Harrison umerekodiwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani tena ndani ya dakika sita kila kitu kilikuwa kimemalizika.

“I’m speechless on this one chris brown komasava certified global anthemworldwide hit diamond platnumz this is big for the culture and for africa we move now … Oya wanangu ni chris brown  kwenye beat ya zombieeeeee put some respect on my name forever.

“NB; this song was made on 27 day of Ramadhan Diamond recorded his part only in 6 minutes god is good allahu albar” S2KIZZ ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hii si mara ya kwanza Chris Brown kuvutiwa na wasanii wa Afrika wiki iliyopita kwenye ziara yake ya ‘11:11’ alitumbuiza na kucheza ngoma ya ‘Tshwala Bam’ iliyoimbwa na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Titom aliyomshirikisha Yuppe.

Wimbo wa ‘Komasava’ (Comment Ça Va) unaendelea kupasua anga duniani kutokana na lugha kadhaa kutumika ndani yake.

Kabla ya Chris Brown kufanya Challenge hiyo mtandaoni, mastaa kibao wakiwemo wanasoka wamewahi kufanya pia na kuweka kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii akiwemo Swae Lee kutokea kundi la Rae Sremmurd, Maitre Gims kutokea Ufaransa, Paul Pogba na wengine kibao.

Share: