Wasanii whozu, bilnas na mboso watakiwa kulipa faini

Kikao cha kusikiliza rufaa ya Wanamuziki wa Bongofleva nchini Whozu, Bilnas na Mbosso kimefikia maamuzi ya kuwataka wasanii hao walipe faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa nchini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao kilichoongozwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kilichofanyika Novemba 14, 2023 katika Ofisi za Wizara hiyo zilizoko Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambacho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwijuma, Katibu Mkuu Bw. Gerson Msigwa, ambapo Mwanamuziki Whozu ametakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni 5, Bilnas Milioni Moja huku Mboso akitakiwa kulipa milioni Tatu na wote kwa pamoja wamepewa onyo kali na kutakiwa kulipa kwanza faini hiyo kabla ya kuendelea na muziki.

Mhe. Waziri Dkt. Damas Ndumbaro amewaasa wasanii hao na wengine nchini watumie vizuri ubunifu wao na kufuata taratibu zilizoainishwa katika mwongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa nchini.

Share: