Wasanii wa filamu watoa faraja kwa majeruhi wa mafuriko hanang.

"Tumeguswa sana na wenzetu Hanang kuna wengine wamepoteza ndugu zao ni muhimu kutoa faraja na kuwatia moyo wenzetu" Yusuph Mlela

Wasanii Filamu Tanzania wamewatembelea majeruhi wa mafuriko Hanang waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hanang (Tumaini) Mkoani Manyara.

Wakizungumza mara baada ya kuwafariji majeruhi baadhi ya wasanii hao wa filamu akiwemo Yusuph Mlela pamoja na Love Juakali wamesema wameguswa katika kutoa faraja kwa majeruhi Hanang.

“Tumeguswa sana na wenzetu Hanang kuna wengine wamepoteza ndugu zao ni muhimu kutoa faraja na kuwatia moyo wenzetu”amesema Yusuph Mlela.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Hanang Dkt. Peter Marwa ametoa shukrani kwa wasanii hao kutenga muda wao na kuwaona wagonjwa.

“Kumfariji mtu ni kumtia nguvu hivyo ujio wa wasanii hawa ni kuwafuta machozi na mgonjwa anajisikia kuwa na yeye ni wa thamani licha ya changamoto alizopitia”amesema.

Tahadhari katika Msimu wa Mvua zimekuwa zikitolewa ikiwemo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, umuhimu wa kutumia maji yaliyowekewa dawa ya kutibu maji au kuchemsha, umuhimu wa kutumia vyoo, kula chakula kikiwa bado cha moto na kufunika chakula kilichoandaliwa tayari kwa kuliwa na pia kuosha matunda na mbogamboga kwa maji safi na salama yanayotiririka kabla ya kula.

Share: