WANDAAJI WA MISS TANZANIA WAFUTIWA LESENI  NA BASATA

Taarifa tulizo zipata kutoka Basata hizi kuhusiana na waaandaaji wa Shindano Miss Tanzania ,kampuni maarufu ya The look company limited ,Miss Tanzania ilianzishwa mwaka 1967...

Shindano la Miss Tanzania linaandaliwa na kampuni ya The Look Company Limited, ikiongozwa na Basila Mwanukuzi (Miss Tanzania 1998)  Lengo ni kuchagua mwanamke mzuri anayewakilisha vibaya zaidi: uzuri, akili, uongozi, na huduma kwa jamii—ikiwa namwelekeo wa “Beauty with a Purpose”.


Sasa mwaka huu 2025 ,Baraza la Sanaa la Taifa @basata.tanzania limeiondolea sifa kampuni inayoendesha mashindano ya Miss Tanzania kutokana na Kushindwa kuhuisha kibali cha kufanya kazi za sanaa kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila sababu ya msingi na pia kukaidi agizo halali la Baraza la kuwasilisha nyaraka hususani nakala ya cheti/leseni ya kushiriki shindano la urembo wa Dunia, pamoja na Kushindwa kufanya shindano la urembo kwa mwaka 2023/2024 na kushindwa kumpeleka Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la urembo wa Dunia kwa mwaka 2024/2025 bila sababu za msingi.


Maamuzi yote hayo yametokana na ukiukwaji wa kanuni ya 39 (g na f) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018, hivyo Baraza limefikia uamuzi wa kumuondolea sifa za kuendesha shindano la Miss Tanzania na kwamba kwa mujinu wa sheria kampuni hiyo ina haki ya kukata rufaa kwa Waziri husika.



Share: