Wanaume wanaachwa nyuma kwenye suala la 'afya ya akili'

"Mara nyingi wanaume wanaachwa nyuma katika masuala ya afya ya akili kutokana na matarajio ya kijamii na dhana potofu zinazohusiana na uwanaume. Kuna picha imewekwa kwenye nyuso za jamii zetu inayowafanya wanaume kushindwa kujieleza kikamilifu au kutafuta msaada kwa matatizo ya afya ya akili pale inapobidi.

"Aidha, mila na desturi za kijinsia zinaweza kuzuia wanaume kushughulikia hisia zao, hivyo kupelekea wanaume wengi kutokupata msaada wa afya ya akili kwa wakati sahihi kulinganisha na wanawake ambao wamekuwa wakiwekewa mazingira mepesi ya kufunguka na kuzungumza kile kinachowasibu.

"Kujenga ujumuishi kwa pande zote mbili katika kushughulikia afya ya akili, tunahitaji kuikosoa dhana potofu, kutoa elimu, na kuunda mazingira salama kwa mazungumzo ya wazi. Huduma za msaada zilizobadilishwa zinapaswa kupatikana, unyanyapaa lazima upunguzwe, na mabadiliko ya kitamaduni yanayowapa watu nafasi ya kuzungumza kile wanachohisi mioyoni mwao yawe yanahimizwa.

Kwa kutoa kipaumbele kwenye ujumuishaji, usawa na uelewa kwa watu wote, tunaweza kushughulikia vizuri matatizo ya afya ya akili kati ya jinsia zote" ameandika @tracy.nabukeera Miss TZ 2023.

Share: