Tyla ametangaza kuhusu mpango wake wa kuachia albamu yake ya kwanza machi 22, 2024

Mwimbaji kutoka Afrika Kusini aliyepata mafanikio makubwa duniani kupitia wimbo wake wa 'Water' Tyla, ametangaza kuhusu mpango wake wa kuachia albamu yake ya kwanza itakayoshirikisha mastaa wakubwa Afrika na duniani kwa ujumla.

Albamu hiyo ambayo itaitwa jina lake ‘TYLA’ imepangwa kuachiwa Ijumaa, Machi 22, 2024 ambapo Tyla kwa mara ya kwanza amepanga kuwashirikisha wakali wakiwemo, mwimbaji maarufu wa R&B, Tems (Nigeria), mkali wa Hip Hop Gunna (Marekani), mwimbaji Skillbeng (Jamaica) na Rapa mwenye Grammy Travis Scott (Marekani) ikiwa na nyimbo 14

Ungependa kuona Album ya msanii gani kutoka Tanzania ikitoka Mwaka huu?

Share: