Tyla amefikia idadi ya wasikilizaji wapatao milioni 30.1 kila mwezi kwenye spotify akimpita rema kutoka nigeria.

Mwimbaji maarufu kutoka Afrika Kusini, Tyla, amesherehekea mafanikio mapya baada ya kuwa msanii wa Afrika mwenye wasikilizaji wengi zaidi kila mwezi kwenye jukwaa la muziki la Spotify, akimpita Rema kutoka Nigeria.

Tyla, ambaye ni moja ya vipaji vipya vinavyochipukia katika tasnia ya muziki wa Afrika Kusini, amefikia idadi ya wasikilizaji wapatao milioni 30.1 kila mwezi kwenye Spotify. Hii ni idadi kubwa ikilinganishwa na msanii Rema kutoka Nigeria, ambaye awali alikuwa na idadi ya wasikilizaji milioni 29.7 kila mwezi.

Hata hivyo, ushindani mkali kati ya wasanii hawa wawili kutoka Afrika Kusini na Nigeria unaonyesha jinsi tasnia ya muziki barani Afrika inavyokuwa na vipaji vingi na ushindani wa kimataifa.

Share: