Trevor noah ashinda tuzo za emmy mfululizo

Kwa ushindi huo, Noah anaweka historia kama Mwafrika wa kwanza na mtu mweusi wa kwanza kushinda Emmy kwa mfululizo bora wa mazungumzo tangu kuanzishwa kwa kitengo hicho mwaka wa 2015.

Mchekeshaji kutoka Afrika Kusini Trevor Noah ameshinda tuzo ya Emmy katika kitengo bora cha mfululizo wa mazungumzo kwa kipindi chake cha mazungumzo The Daily Show.

Kwa ushindi huo, Noah anaweka historia kama Mwafrika wa kwanza na mtu mweusi wa kwanza kushinda Emmy kwa mfululizo bora wa mazungumzo tangu kuanzishwa kwa kitengo hicho mwaka wa 2015.

"Inashangaza kwamba ninapata kuwa sehemu ya safari hii. Ninahisi kama kuwa sehemu ya timu ya soka iliyoshinda," Noah alisema baada ya kupata ushindi huo Jumatatu usiku.

Mchekeshaji huyo aliwahi kuteuliwa kuwania kitengo cha Emmy mara tano hapo awali, lakini uteuzi wake wa sita, ambao aliupata katika msimu wake wa mwisho akiandaa kipindi cha The Daily Show, hatimaye ulimwezesha kushinda.

Mnamo Septemba 2022, Noah alishangaza mashabiki wake wengi alipotangaza kujiondoa kwenye The Daily Show, baada ya miaka saba kama mtangazaji.

Shughuli ya kumtafuta atakayechukua nafasi yake bado inaendelea, Noah ana tuzo nyingine ya Emmy ambayo alipata mwaka wa 2017, Tuzo za Emmy ni tuzo za kifahari zaidi katika tasnia ya runinga ya Amerika.

Share: