Tiktok yaanza kuondoa miziki iliyo chini ya lebo ya universal music

TikTok inasema imeanza kuondoa muziki zaidi kwenye jukwaa lake kuhusiana na mzozo unaoendelea kuhusu mirahaba na Universal Music Group (UMG).

Programu hiyo tayari imezima nyimbo za wasanii waliosainiwa na lebo, lakini sasa inapaswa kufanya vivyo hivyo na waandishi pia.

Hii inamaanisha kuwa video zinazoangazia nyimbo za wasanii kama vile Harry Styles na Adele, ambao wameandika na wasanii waliosainiwa na Universal, zinaweza kuzimwa hivi karibuni.

TikTok inasema hadi 30% ya nyimbo inazoziita "nyimbo maarufu" zinaweza kupotea.

Lakini makadirio mengine katika ya tasnia hiyo yanasema hadi 80% ya muziki wote kwenye TikTok unaweza kuzimwa.

Hiyo ni kwa sababu ya kitu kinachoitwa "hakimiliki zilizogawanyika".Hatua inamaanisha ikiwa mtunzi aliyetia saini kwenye kitengo cha uchapishaji cha Universal Music amechangia hata sehemu ndogo kwenye wimbo, rekodi hiyo yote, kwa nadharia, itabidi ishushwe.

Hiyo itajumuisha nyimbo za wasanii kwenye lebo zingine, zikiwemo nyimbo kuu mbili zilizosalia, Sony na Warner, na mamia ya watu huru.

Share: