TAYLOR SWIFT ATANGAZA UCHUMBA NA TRAVIS KELCE

Mwanamuziki maarufu Taylor Swift ametangaza kuchumbiwa na mpenzi wake ambaye ni mchezaji wa Kansas City Chiefs, Travis Kelce.

Taylor Swift ametangaza habari hiyo kupitia chapisho la kwenye Instagram, akiandika: "Mwalimu wako wa Kiingereza na mwalimu wako wa mazoezi ya viungo wanafunga ndoa."

Tangazo hilo lilipata likes zaidi ya milioni 1.7 ndani ya dakika 30 tu baada ya kupostiwa.

Swift na Kelce walianza uhusiano wao mwaka 2023, baada ya bingwa huyo mara tatu wa Super Bowl kusema katika podcast yake New Heights kwamba alijaribu bila mafanikio kukutana na mwimbaji huyo kwenye tamasha lake la Eras Tour huko Kansas City.

Uvumi ulianza kuenea kwamba wawili hao walikuwa wakichumbiana baada ya Swift kuonekana kwenye mechi kadhaa za Chiefs. Katika mara yake ya saba kushuhudia mchezo akiwa jukwaani, alifika akiwa na baba yake, Scott Kingsley Swift.

Share: