Taylor swift amejitokeza kumuunga mkono lady gaga Baada ya kukanusha uvumi wa ujauzito

Taylor Swift amejitokeza kumuunga mkono Lady Gaga, ambaye alichapisha video akikanusha uvumi wa ujauzito, kwa kuita maoni kuhusu hilo "ya kuvamia na kutowajibika".

Waimbaji hao wawili mashuhuri wa Marekani walijibu baada ya uvumi mtandaoni kuwa mwimbaji aliyeshinda tuzo ya Grammy na mshindi wa tuzo ya Oscar Lady Gaga alikuwa mjamzito.

Watu walianza kutoa maoni yao baada ya kuonekana kwa picha za nyota huyo akiwa na mpenzi wake Michael Polansky walipokuwa wakisherehekea harusi ya dadake Natali Germanotta nchini Marekani.

Gaga alichapisha video kwenye TikTok, akirejelea wimbo Down Bad, kutoka kwa albamu mpya ya Swift, akisema: "Not pregnant - just down bad cryin at the gym."

Swift alichapisha chini ya video hiyo: "Je! sote tunaweza kukubaliana kuwa ni uvamizi na kutowajibika kutoa maoni juu ya mwili wa mwanamke.

"Gaga hana mtu yeyote ambaye ni lazima ajieleze kwake na wala mwanamke yeyote yule."

Maoni ya Swift yalisababisha watu wengi kujibu, kama vile "Gaga na Taylor OMG" na mapendekezo ya matumaini kwamba wawili hao wanaweza kufanya ushirikiano wa muziki.

Hii si mara ya kwanza kumekuwa na uvumi mtandaoni kuhusu iwapo mtu mashuhuri ni mjamzito.

Share: