SWAG: JUSTIN BIEBER ACHIA ALBUM MPYA KWA KUSTUKIZA

Nyota mkubwa wa muziki wa pop Justin Bieber ameachia rasmi albamu yake ya saba SWAG kupitia lebo ya Def Jam, ikiwa ni kazi yake ya kwanza tangu Justice ya mwaka 2021.

Albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 21, na inawashirikisha wasanii mbalimbali kama Gunna, Sexxy Red, Cash Cobain, Lil B, Eddie Benjamin na wengine. Baadhi ya majina ya nyimbo kwenye albamu hiyo ni kama “ALL I CAN TAKE,” “STANDING ON BUSINESS,” na “FORGIVENESS.”


Kabla ya kutolewa kwa SWAG, Bieber alishirikisha mashabiki picha za mwanawe akiwa naye ndani ya studio akirekodi. Mnamo Mei, chanzo kingine kilidokeza kuwa Bieber alikuwa akifanya kazi ya muziki katika hoteli ya Eleven Deplar Farm huko Ólafsfjörður, Iceland, ambayo ina studio ya kisasa ya kurekodia iliyo pembeni ya jengo kuu.


Tufuatilie kupitia #STBongoTV ndani ya kisimbuzi cha @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.


#STBongoUPDATES #nyumbanikwanza


Share: