
Super Bowl ni moja ya matamasha makubwa zaidi ya michezo na burudani duniani,, na wasanii wengi wanapata fursa ya kutumbuiza wakati wa mapumziko ya mchezo huo. Lakini kwa nini wasanii hawalipwi moja kwa kutoa burudani kwenye jukwaa hilo?
Kwanza, kuonekana kwenye jukwaa la #SuperBowl ni fursa muhimu ya kujitangaza kwa wasanii. Tamasha hilo linavutia mamilioni ya watazamni duniani, na kuonekana kwenye jukwaa hilo kunaweza kuongeza umaarufu wa msanii na kuleta faida kubwa zaidi kwa muda mrefu. Wasanii wengi hupata faida kupitia kuongezeka kwa mauzo ya nyimbo, matangazo, na fursa za kibiashara baada ya kuonekana kwenye tamasha hilo..
Pili, Shirika la National Football League (#NFL) halilipi wasanii moja kwa moja kwa sababu jukwaa lao linatoa umaarufu mkubwa na nafasi ya kujitangaza kwa wasanii. Badala yake, wasanii hupata faida kwa njia nyingine, kama vile kuongezeka kwa mashabiki (followers, subcribers) na fursa za kibiashara.
Usiku wa kumkia kesho, jukwaa hilo litakuwa na mgeni, Kendrick Lamar. Shoo hiyo itafanyika jijini New Orleans. Watazamaji wanangojea kwa hamu kuona kile ambacho Kendrick ataleta kwenye jukwaa hilo la kimataifa.
Ingawa wasanii hawalipwi moja kwa moja kwa kutumbuiza Super Bowl, fursa za umaarufu na pesa zinazotokana na tamasha hilo mara nyingi huwa na thamani kubwa zaidi. Na kesho, Kendrick Lamar atathibitisha jinsi shoo ya Super Bowl inavyoweza kuwa hatua muhimu kwenye kazi ya msanii.