Stephen Williams adai Serena Wiliams alistahiri talaka kutoka kwa Drake

Mchambuzi wa michezo Stephen A. Smith amesema asingekubali kitendo cha Serena Williams kumtania Drake wakati wa shoo ya Kendrick Lamar kwenye #SuperBowl2025.

Akizungumza kwenye kipindi cha First Take, Smith (57) alisema kama mke wake angefanya hivyo kwa mpenzi wake wa zamani, basi angemwacha mara moja. "Kama uko na mimi, kwanini bado unamuwaza ex wako? Nenda tu kwake!" alisema kwa msisitizo.

Serena Williams (43) aliwashangaza mashabiki wa Super Bowl alipocheza crip-walk wakati #KendrickLamar akiimba wimbo wake wa kumdiss Drake, #NotLikeUs. Tukio hilo limechukuliwa kama shambulio jingine kwa rapa huyo wa Canada.

Ingawa Serena Williams na Drake hawakuwahi kuthibitisha uhusiano wao, walihusishwa kimapenzi kati ya 2011 na 2015. Drake aliwahi kumtaja Serena kwenye wimbo wake wa 2013 Worst Behavior na kudai aliandika Too Good kuhusu Serena.

Share: