Baada ya kusambaa kwa taarifa za Shilole na Mume wake Rommy 3D kuachana kwenye mitandao ya kijamii Rommy amejitokeza na kuweka wazi kila ambacho kinaendelea kwenye ndoa yao
Rommy ameshare picha akiwa na Shilole na kuisindikiza na ujumbe ambao moja kwa moja unaonekana kuthibitisha kuwa ni kweli yeye na mke wake hawako pamoja tena
Rommy ameandika "Habari Ndugu zangu kama ambavyo mmeona kwenye mitandao na hiyo ndio hali halisi basi Mimi na aliyekuwa mwenzangu Zuwena Mohamed (Shilole)"
"Naona tumefikia Mwisho na si Vibaya nikakubali matokeo na kumpisha Kijana mwenzangu aendeleze gurudumu hili, na Maisha yaendelee... nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa vile tulivyoishi siku zote za mapenzi yetu, Wabillah Tawfiq
Share: