
A$AP Rocky anaweza kuwa na albamu mpya njiani, lakini kwa sasa, inaonekana kuwa kipaumbele chake kikuu ni familia. Huku yeye na Rihanna wakijiandaa kumkaribisha mtoto wao wa tatu.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wawili hao, uhusiano wa Rocky na Rihanna umeimarika zaidi tangu walipoanza kuwa wazazi. Wana watoto wawili tayari: RZA Athelston na Riot Rose, na inasemekana walikuwa na mpango wa kuwa na watoto wa karibu umri ili wajenge uhusiano wa kindugu wa karibu wakiwa wadogo.
Rocky anaelezewa kama baba anayehusika kikamilifu—akishughulikia mambo ya usiku kama kulala watoto, kazi za nyumbani, na kuhakikisha Rihanna anapata mapumziko anayohitaji.
Kwa upande mwingine, ingawa maisha yao ya kifamilia yanaonekana kustawi, mashabiki bado wanasubiri kwa hamu albamu ya A$AP Rocky iitwayo DON’T BE DUMB, ambayo imecheleweshwa kwa muda mrefu. Pia, Rihanna hajarejea rasmi kwenye muziki, licha ya matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki wake ambao kwa miaka kadhaa sasa wanaisubiri album yake ya tisa.
Tufatilie kupitia kisumbuzi @startimestz CH 161 (antena) CH 401 (Dish) pamoja na kwenye YouTube channel yetu ya #STBongoTV Kwa Taarifa zaidi.
#STBongoUpdates #NyumbaniKwanza