Rapper meek mill autaka uraia wa ghana

Rapper kutoka Marekani meek mill amefunguka kutamani kuchukua uraia wa Ghana, Meek amesema anautaka uraia wa Ghana kwani amechoshwa na tabia ya Wamarekani kuwadidimiza watu weusi kama wasipofuata maagizo

Kupitia ukurasa wake wa X aliandika “Ninataka kupata Uraia wa Ghana, Marekani imetengenezwa kwa ajili ya kuwadidimiza Wanaume Weusi kama usipofata maagizo.”

Hivi karibuni Meek amekuwa akigonga vichwa vya habari baada ya kuhusishwa katika sakata la diddy la kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja na yeye akiwa moja ya wahhukiwa wa sakata hilo.

Share: