Rapa moni centrozone kumaliza tofauti zake na msanii mkongwe q chief

Rapa Moni Centrozone ameweka wazi kumaliza tofauti zake na mkongwe wa muziki q chief ambaye walifanya pamoja project ya Dr Malume kazi iliyotoka miezi kumi iliyopita


Kwa mujibu wa Moni Centrozone Q chief ambaye alifanya chorus kwenye wimbo huo hakupendezwa na namna ambavyo Moni aliitoa Project hiyo ambayo alimshirikisha

Moni ameshare DM ambayo ametumiwa na Q chief kuhusuania na kukunjua roho kwake na kumtakia kila lenye heri kwenye kazi zake hususani hii mpya ambayo anaifanyia Promotion kwa sasa

Share: