Rapa 50 cent amemshtaki ex wake daphne joy kwa madai ya kumchafua na kumdhalilisha

Wakati sakata la rapa 50 Cent la kutaka achukue jukumu la Malezi Ya mtoto wake Kwa Muda Wote likiendelea mahakamani, rapa huyo amemshtaki pia Ex Wake Daphne Joy, kwa madai ya kumchafua na kumdhalilisha.

Cent anadai kuwa Baby Mama wake huyo amemchafua pale Alipodai kuwa alibakwa na kunyanyaswa kingono na 50 Cent.

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama Zilizodakwa Na Tovuti Ya ‘Us Weekly’ jana Jumannne; Rapa 50 Cent amedai kuwa Joy ametoa shutuma za uongo tena hadharani (Falsely & Publicly).

Hayo yote yameibuka baada ya hivi karibuni mtayarishaji Rodney Jones, kufungua kesi ya unyanyasaji dhidi ya Diddy na kumtaja Daphne, kama mmoja kati ya wanawake waliokuwa wanajiuza kwa Diddy, kitendo ambacho kiliibua vita ya maneno kati ya 50 na Baby Mama wake akimuita kuwa ni ‘Changudoa mdogo’ huku yeye akishutumiwa kuwahi kumbaka na kumnyanyasa kingono wakati wa mahusiano yao mwaka 2011 - 2013.

Share: