Ziara yake ya Korea Kusini aliyofuatana na wasanii wa maigizo ni mfano halisi wa upendo wa mama kwa wanawe wasanii.
Ipo haja ya taasisi nyingine za serikali anazoziongoza ziongeze juhudi katika kumuunga mkono katika harakati hizi.
Nitatolea mfano Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), ambayo ndiyo national carrier yaani ndiyo mbeba bendera wa taifa.
Ukipanda ndege za ATC ni vyema ukajiona umepanda ndege ya kampuni ya nyumbani na sio ya nchi za mbali huko.
Kampuni nyingine za ndege huweka kazi za sanaa za wasanii wao kama kiburudisho kwa abiria, hasa kwa safari ndefu.
Nasi kampuni yetu inaweza kututangaza katika hili. Ni vyema nyimbo za wanamuziki wa Tanzania na filamu za waigizaji wa Tanzania zipewe nafasi.
Share: