Rais samia awapongeza ramadhani brothers

Rais Samia amewapongeza Vijana wa Tanzania Ramadhani brothers baada ya kufanikiwa kushinda shindano la America’s Got Talent Fantasy League lililofanyika huko nchini Marekani. Ramadhani Brothers wameweka rekodi ya kuwa Waafrika wa kwanza kushinda AGT.

“Pongezi kwa vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League. Safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine. “

Share: