Rais mhe. samia suluhu amekutana na mwanamuziki maarufu nchini korea, bw. cho yong-pil

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na Mwanamuziki maarufu nchini Korea, Bw. Cho Yong-pil ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii. 

Bw. Cho ambaye yupo katika fani ya muziki kwa zaidi ya miaka 50 anaelezwa kuwa ni mmoja wa Wanamuziki nguli, wenye ushawishi mkubwa nchini Korea aliyeshinda tuzo mbalimbali kupitia kampuni ya YPC. 


Bw. Cho ambaye ameimba nyimbo mbili kuhusu Tanzania, “Leopard of Kilimannjaro na Like Serengeti” alimweleza Rais Samia kuwa anaipenda Tanzania na anatamani kufika nchi hiyo kwa mara ya pili kabla hajaondoka hapa duniani. 

Rais Samia alimshukuru Bw. Cho kwa nyimbo zake hizo ambazo kutokana na umaarufu wake zimeitangaza Tanzania sio tu Korea bali duniani kote, na kumsihi arejee Tanzania ili atunge nyimbo kuhusu vivutio mbalimbali vya utalii na utamaduni.

Share: