
Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amejubu baada ya video yake kusambaa akiwashauri wananchi kujituma badala ya kulalamikia serikali.
Video hiyo ambayo imesambaa kwa kasi mitandaoni imekosolewa vikali na watu mbalimbali wakidai kuwa nyota huyo wa muziki ameongea kwa dharau, Diamond kupitia Instagram yake amejibu tuhuma hizo kwa kuandika;
"Najua kwa akili ya haraka unaweza ona jamaa jau, ila sikiliza ukweli mchungu toka kwa Mpambanaji Mwenzio... Skiliza huu ukweli ambao walofanikiwa hawakuambii ukweli wanakutumia tu kwenye agenda... Fahamu ya kua wote
Unawaona hapo Kuanzia Viongozi Wapinzani hadi Viongozi wa Madarakani wote wapo kazini kwao, yani hapo wanachokifanya ni Kazi, na tunachojadili hapa ni Kazi zao... Wamepambana kila mmoja kwa namna yake Hadi kufanikiwa kupata nafasi hizo... hivyo jua kwamba wenzako unaowajadili hapo, kwanza kabisa wako Kazini hapo, wanafanya kazi...kwa imani yako wewe unamuona pengine labda Mpinzani eti anauchungu sana na wewe, Hapana hio ni kazi yake na ni njia yake ya kutafta rizki ....wote wapo kazini wanachokifanya ni kazi, yani hio ni njia yake ya yeye kutengeneza mkate na kutimiza ndoto zake pia za kiuongozi, hivyo amka kaka, Kimbizia nawe ndoto zako, tafta na wewe namna ya kupambana Kutafta Mkate ndugu, jua kwamba Mkombozi Mkuu wa Maisha yako ni Wewe kwa kupambana na kutafta fursa mbalimbali kwanza, na Amini ya kwamba fursa zipo na kama kweli wewe sio bishoo mchagua kazi, na Unania, Juhudi na una uwezo wa kuifanyia kazi hio fursa, basi Ukizitafuta na Kumuomba Mwenyez Mungu atakubariki ata
kama itachelewa kwa Muda ila one day itakuja tu” Diamond ameandika.
“Of course, Kama kijana mwenye akili siamini kuwa kila linalosemwa halina tija, ila ushauri wangu usibebe kila unachoambiwa, usikubali kufanywa mjinga ukaacha kufocus kujenga Maisha yako na Familia yako ukafata Mikumbo ya watu ambao wao wanafanya kazi na kuishi Maisha yao mazuri tena Wengine wako nje ya nchi na Familia zao wanaenjoy life halaf wakataka kukuingiza wewe Mkenge Upate Ukilema ibaki familia yako ndio inasononeka! Amka Babu!!! Hao wenyewe wanaokushawishi ujinga hapo wapo kazini ujue, kuna ambao Washalipwa, Kuna Ambao wanapambana Kutimiza ndoto, na Kuna wenye hasira ya Kuwa wamepoteza Mkate wa Mwanzo!! Amka kaka” Aliongeza.