PICHA ; TRUMP AWAALIKA IKULU MABONDIA WA UFC

Rais wa Marekani, Donald Trump, amefunguka kuhusu mpango wake wa kuusogeza ‘White House’ mchezo wa Sanaa ya Mapigano Mchanganyiko (UFC), akiwa amedhamiria kufanya hivyo mwakani (2026) katika sherehe za Miaka 250 ya Uhuru wa Marekani.

Trump ni shabiki mkubwa wa mchezo huo na amewahakikishia waratibu wa UFC kwamba atawapa eneo la kutosha litakalowawezesha kutengeneza jukwaa rasmi kwa ajili ya mabondia sambamba na watazamaji.


Rais Trump alishawahi kuonekana katika mapambano kadhaa ya UFC miaka ya hivi karibuni na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki alioungana nao, huku mabondia wa mchezo huo pia walimpongeza kwa wingi kufuatia ushindi wake kwenye kinyang’anyiro cha Urais.


Share: