Peter morgan wa kundi la heritage afariki dunia

Peter Anthony Morgan, mwimbaji kiongozi wa Morgan Heritage, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 47. Familia ilitangaza kifo chake siku ya Jumapili ingawa mpaka sasa chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi.

"Kwa upendo wa dhati tunawataarifu kwamba mpendwa wetu mume, baba, mtoto na kaka na mwimbaji kiongozi wa Morgan Heritage (Peter Anthony Morgan) amefariki dunia leo Februari 25, 2024. Mungu njoo utuokoe kutoka kwetu kwa sababu upendo ndio njia pekee. ," lilisomeka andiko hilo.

"Familia yetu inakushukuru kwa upendo wako mwingi na msaada wako na tunaomba maombi yako endelevu wakati tunapopitia mchakato huu. Tunakuomba uheshimu faragha yetu wakati huu wa maombolezo. Asante!"

Share: