
Katika maendeleo mapya ya kesi dhidi ya rapa maarufu Sean “Diddy” Combs, waendesha mashtaka wametangaza kwamba hawataendelea na mashtaka matatu kati ya yale aliyokuwa akikabiliwa nayo.
Hivi sasa Sean "Diddy" Combs (Sean Combs) anakabiliwa na mashtaka makubwa ya jinai katika mahakama ya Marekani.
Mashtaka Makuu
Racketeering Conspiracy
Kuingiliana katika mpangilio wa jinai ("criminal enterprise"), unaodaiwa kujumuisha ugaidi, rushwa, utekaji nyara, kulipiza kisasi kwa moto, na uharibifu mwingine .
Inaweza kusababisha adhabu ya maisha ya kifungo.
Sex Trafficking by Force, Fraud, or Coercion
Kuna mashtaka mawili tofauti ya kusafirisha na kumtumbukiza mtu katika ukahaba au masuala ya ngono kwa kutumia nguvu, udanganyifu au tishio,Adhabu ya mwaka angalau 15, ikiwa atapatikana na hatia
Transportation to Engage in Prostitution
Mashtaka mawili yanamlenga kusafirisha watu kwa ajili ya ukahaba, chini ya sheria ya Mann Act.
Sasa Mashtaka yaliyofutwa ni Jaribio la utekaji nyara (attempted kidnapping), Jaribio la kuanzisha moto kwa makusudi (attempted arson) na Kusaidia na kushirikiana katika usafirishaji wa binadamu kwa madhumuni ya ngono (aiding and abetting sex trafficking).
Tangazo hilo lilitolewa Jumanne kupitia barua rasmi kwa jaji. Waendesha mashtaka wamesema wameamua kuyaondoa mashtaka hayo ili kuiwezesha jury (baraza la mahakimu) kuelewa kesi kwa urahisi zaidi.
Baada ya tangazo hilo, mawakili wa Diddy waliomba kesi itupiliwe mbali kabisa, wakisema upande wa mashtaka umeshindwa kutoa ushahidi madhubuti hata kwa mashtaka yaliyosalia.