Onyesho la kenya la koffi olomide katika hali ya sintofahamu juu ya madeni

Nsana Productions, Mapromota au wahamasishaji wanasema nyota huyo wa rumba mwenye umri wa miaka 67 alikiuka masharti ya kandarasi ya tamasha la Machi 2016 ambapo wanataka kurejeshewa dola 65,000 (£52,000).

Mapromota wa muziki wanatishia kutatiza tamasha kubwa la mwimbaji wa Kongo Koffi Olomide lililopangwa kufanyika nchini Kenya siku ya Jumamosi kwa sababu ya deni la 2016.

Nsana Productions, Mapromota au wahamasishaji wanasema nyota huyo wa rumba mwenye umri wa miaka 67 alikiuka masharti ya kandarasi ya tamasha la Machi 2016 ambapo wanataka kurejeshewa dola 65,000 (£52,000).

Olomide alizuiwa mwaka 2016 kutumbuiza na kufukuzwa Kenya kwa madai ya kumpiga mmoja wa wacheza densi wake wa kike. Picha za tukio hilo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Nairobi ziliwekwa mtandaoni na kuzua taharuki kwenye mitandao ya kijamii.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwimbaji huyo kurudi kutumbuiza nchini Kenya baada ya tukio hilo.

Kupitia kwa mawakili wake, Olomide amewahakikishia mashabiki wake kuwa tamasha hilo la amani linalosubiriwa kwa hamu litaendelea licha ya vitisho kutoka kwa mapromota.

Mratibu wa hafla hiyo anasema kuwa mafanikio ya tamasha hilo hayataathiriwa.

Akizungumza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) siku ya Jumatano muda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya, Olomide alisema amewakosa mashabiki wake wa Kenya ambao aliwaahidi onyesho la kuvutia.

Share: