Aderinoye Queen Christmas, anayejulikana pia kama Malkia Oluwadamilola Aderinoye, anasemekana kawatoroka maofisa wa Shirika la Kitaifa la Kupambana na Dawa za Kulevya (NDLEA) walipovamia makazi yake huko Lagos wiki jana.
Mamlaka nchini Nigeria imetangaza kuwa malkia wa zamani wa urembo anasakwa kwa madai ya kuhusika na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Aderinoye Queen Christmas, anayejulikana pia kama Malkia Oluwadamilola Aderinoye, anasemekana kawatoroka maofisa wa Shirika la Kitaifa la Kupambana na Dawa za Kulevya (NDLEA) walipovamia makazi yake huko Lagos wiki jana.
Shirika la kupambana na unyanyasaji wa dawa za kulevya katika taarifa lilisema uvamizi huo ulifuata "intelijensia" ya kuaminika kwamba malkia huyo wa zamani wa urembo alihusika katika dawa haramu.
"Zilizopatikana kutoka nyumbani kwake wakati wa msako ulioshuhudiwa na maafisa wanaohusika na masuala ya mali ni pamoja na gramu 606 za Canadian Loud, aina ya bangi, mizani ya kielektroniki, idadi kubwa ya plastiki zinazopakiwa dawa," taarifa hiyo iliongeza.
Mshukiwa huyo alikuwa Miss Commonwealth Nigeria Culture 2015/2016 na mwanzilishi wa Queen Christmas Foundation.
Bado hajatoa maoni yake kuhusu tuhuma hiyo.
Mshukiwa mwingine, ambaye alikuwa akirejea kutoka Brazil wiki jana, pia alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed kwa kumeza vidonge 60 vya kokeini, shirika hilo lilisema.