Naomba radhi watanzania kwa kilichotokea

Star wars Muziki wa Bongo Fleva zuchu ameomba Radhi kwa Mashabiki zake na Baraza la Sanaa la Taifa Kwa Kile Kilichotokea Katika Show yake ya Zanzibar Tarehe 24 February

Baraza la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, Limemfungia zuchu kutokufanya shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar na Kupiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita

Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika show ya full moon party zanzibar - Kendwa anadaiwa kutumia lugha na ishara Mbaya zinazokiuka maadili ya Zanzibar

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Tsh. milioni 1 kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.

Share: