NAIGIZA TU ILA HUWA SIANGALII FILAMU KABISA - DENZEL WASHNGTON

Denzel Washington huenda akawa mwigizaji mahiri zaidi wa kizazi chake, lakini jambo la kushangaza ni kwamba hana hamasa ya kuangalia filamu.

Katika mahojiano mapya na A$AP Rocky na Spike Lee kwa jarida la GQ, mshindi huyo wa Oscar mara mbili alifichua ukweli huo:

"Siiangalii filamu, kaka. Kweli kabisa. Siiendi kwenye sinema, siiangalii filamu," alisema Washington.

Rocky alipomuuliza kama ni kwa sababu amecheza filamu nyingi kiasi cha kuchoshwa nazo, Denzel alijibu kwa kifupi:


"Huenda. Najua nimechoka na filamu."

Lakini ingawa haangalii sinema, Denzel aliweka wazi upande mwingine anaoutumia kupata burudani — Muziki wa rap.

Vile vile A$AP Rocky alifichua kupitia Million Dollaz Worth Of Game kuwa alipokuwa setini, alishiriki rap battle na Washington:

"Nilishtuka sana kuona jamaa ni shabiki mkubwa wa hip-hop. Nilidhani yupo kwenye jazz ya Miles Davis au Coltrane. Lakini ghafla akaanza kutupa mistari ya Moneybagg Yo, NLE Choppa na DMX. Alianza kufreestyle tu kama kawaida, na ukweli ni kwamba alinitoa nishai — nilishindwa battle na Denzel," alisema Rocky akicheka.

Share: