kumfanyia mahojiano na kumuweka kwenye cover ni kwasababu ya kazi ambazo anazifanya, kwanza kama Model lakini pia kwa kazi anazozifanya kupitia Foundation yake Flaviana Matata Foundation
Mwanamitindo Flaviana Matata na Mkurugenzi wa Taasisi ya Flaviana Matata Foundation, amelipamba jarida maarufu la Hamptons kwenye cover ambapo humo ndani ameelezea maisha yake na jinsi anavyotumia ushawishi wake kutoa mchango kwenye Nchi yake ya Tanzania kupitia Taasisi yake ikiwemo kusomesha watoto wa kike wanaotoka kwenye mazingira magumu, kugawa pedi kwenye shule mbalimbali na kujenga vyoo, maji na vyumba maalumu kwa ajili ya Wasichana kujisitiri wakiwa kwenye siku zao za hedhi.
Flaviana amemwambia Millard Ayo kuwa Jarida hilo lilishawishika kumtafuta, kumfanyia mahojiano na kumuweka kwenye cover ni kwasababu ya kazi ambazo anazifanya, kwanza kama Model lakini pia kwa kazi anazozifanya kupitia Foundation yake Flaviana Matata Foundation
“Hili toleo la cover ni gazeti ambalo linatolewa kila wakati wa majira ya joto, wakaifanya habari yangu kwa kutumia Foundation yangu na kuangazia Mimi kama Model kwa namna gani natumia platform yangu kufanya mambo ya kimaendeleo sehemu niliyotoka Tanzania” - Flaviana Matata.
Kwa mujibu wa Wikipedia, Hamptons ni jarida lililoanzishwa Nchini Marekani na Randy Schindler mwaka 1978 na huchapishwa mara 13 kwa mwaka likiangazia masuala mbalimbali ikiwemo fashion, utamaduni, ubunifu na mengineyo.
Share: