Akiongelea juu ya mafanikio ya muziki huo, Rayvanny ameipongeza kazi ya Msanii Misso Misondo na kikundi chake kwa kuteka soko la TikTok
Katika mahojiano na kipindi cha 3 shots of tequila, kilichofanyika nchini Uingereza, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny, amezungumzia umuhimu wa muziki wa Singeli kutoka Tanzania katika soko la kimataifa. Rayvanny amesisitiza kuwa ni wakati wa ulimwengu kusikiliza muziki wa Afrika, hususan Singeli, ambao unachipuka na kufurahisha watu kwa mtindo wake wa kipekee.
Akiongelea juu ya mafanikio ya muziki huo, Rayvanny ameipongeza kazi ya Msanii Misso Misondo na kikundi chake kwa kuteka soko la TikTok na kueneza vibe lao la kipekee. Amesifia uwezo wao wa kubuni mitindo ya kucheza inayovutia na kuwaleta pamoja watazamaji wa kimataifa. Rayvanny pia amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na vijana wenye vipaji ili kukuza tasnia ya muziki kwa ujumla.
Kufuatia mazungumzo hayo, muziki wa Singeli unatarajiwa kuvuma zaidi katika jukwaa la kimataifa, huku wasanii kama Misso_Misondo wakiendelea kung'ara na kuhamasisha maendeleo ya muziki wa Tanzania.