Muigizaji andre braugher amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61

Andre Braugher, nyota wa Brooklyn Nine-Nine, Homicide: Life on the Street, Men of a Some Age and Glory amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Kifo cha mwigizaji huyo wa Marekani kilithibitishwa na maajenti wake, ambao walisema kwamba kilikuja baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Braugher mara nyingi aaliigiza kama afisa wa polisi wakati wa kazi yake, akiigiza katika majukumu ya kuigiza na ya ucheshi.

Mzaliwa wa Chicago, alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Stanford kabla ya kuhudhuria Shule ya Juilliard kwa michezo ya kuigiza.

Braugher alicheza kama mwanajeshi wa Muungano ambaye anajiunga na kikosi cha Wamarekani Weusi katika filamu ya 1989 ya Glory - filamu ambayo ilishinda tuzo ya mwigizaji msaidizi bora ya Oscar kwa mwigizaji mwenzake Denzel Washington.

Kazi ya Baugher ilisifiwa sana katika filamu ya Homicide akicheza kama mpelelezi Frank Pembleton. Akiongea na BBC News mapema mwaka huu , mwandishi na mtayarishaji wa Homicide Tom Fontana alisifu uwepo wake wa skrini unayovutia, unayoangazia haiba na msisimko.

"Sijawahi kuona mwigizaji kama huyo kwenye televisheni," alisema Bw Fontana."

Share: